Rais wa Iran ahimiza kuimarisha sekta binafsi ili kuvutia mitaji ya kigeni
2021-05-17 08:54:02| CRI

Rais Hassan Rouhani wa Iran amehimiza kujenga “usalama wa kiuchumi” kwenye sekta binafsi, ili kuvutia zaidi uwekezaji wa kigeni katika maeneo yake maalumu ya kiuchumi na biashara huria.

Kwenye mkutano wa Makao Makuu ya Uratibu wa Kiuchumi uliofanyika Tehran, rais Rouhani amesema upanuzi wa shughuli za kiuchumi kwenye maeneo ya biashara huria ya Iran unahitaji kujenga imani na unyumbufu ili kuchukua sehemu kubwa zaidi katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Pia amesema sera za mambo ya nje zinatakiwa kuweka msingi kwa ajili ya kuondolewa kwa vizuizi vikuu ili kuvutia mitaji ya kigeni.