Hotuba ya rais wa China kuhusu kumalizika kwa umasikini uliokithiri yachapishwa kwa lugha ya Kiingereza
2021-05-17 09:20:18| CRI

Hotuba ya rais Xi Jinping wa China katika mkutano wa kuadhimisha mafanikio ya nchi hiyo katika kutokomeza umasikini na kutoa tuzo kwa watu waliokuwa mfano wa kuigwa katika mapambano hayo imechapishwa kwa lugha ya Kiingereza.

Hotuba hiyo iliyotolewa mwezi Februari na rais Xi akitangaza kuwa China imepata ushindi kamili katika kukabiliana na umasikini, imetafsiriwa na Taasisi ya Utafiti wa Historia na Nyaraka za CPC.

Katika hotuba hiyo, rais Xi ametaka juhudi zaidi ili kuendeleza kwa pande zote ufufukaji wa maeneo ya vijijini na kuongeza mafaniko yaliyopatikana katika kuondokana na umasikini.