Mabalozi wa China, Norway na Tunisia kwenye UM watoa taarifa ya pamoja kuhusu suala la Palestina na Israel
2021-05-17 09:49:08| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun pamoja na wajumbe wa kudumu wa Norway na Tunisia walikutana na waandishi wa habari kwa pamoja baada ya mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel, na kutoa taarifa ya pamoja kuhusu suala hilo.

Mabalozi hao wameeleza kufuatilia kwa karibu  hali ya Gaza na kuongezeka kwa idadi ya vifo na majeruhi, wakisisitiza kusimamisha mapigano mara moja, kutekeleza sheria za kimataifa ikiwemo sheria ya kibinadamu ya kimataifa, na kuwalinda raia hasa watoto.

Wamesisitiza kuunga mkono pande hizo mbili kufikia ufumbuzi wa nchi mbili kwa njia ya mazungumzo, kwa mujibu wa maazimio husika ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, na pia wametoa wito wa kuimarisha na kuharakisha juhudi za diplomasia ili kutimiza lengo hilo.