Watu wawili wafariki baada ya mabenchi ya sinagogi la wayahudi kuvunjika huko Ukingo wa Magharibi
2021-05-17 08:56:20| CRI

Watu wawili wamefariki na wengine wapatao 160 wamejeruhiwa baada ya mabenchi kwenye sinagogi moja la wayahudi lililoko katika eneo la makazi ya wayahudi ukingo wa magharibi kuvunjika jana usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi wa Israel, tukio hilo lilitokea wakati waumini wapatao mia sita wa Kiyahudi walipokusanyika kwenye sinagogi moja ambalo ujenzi wake bado haujakamilika.