Iran yakanusha kuwa “kuna makubaliano ya awali” kwenye mazungumzo ya Vienna
2021-05-17 19:39:48| CRI

 

 

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imekanusha kuwa “kuna makubaliano ya awali” kwenye mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna kuhusu kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 (JCPOA).

Akiongea kwenye mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Saeed Khatibzadeh, amesema hakuna kitu kama makubaliano ya awali, na hakuna makubaliano yatakayofikiwa hadi matakwa yote yatakapotimizwa. Amesema mazungumzo yanaendelea na sehemu muhimu ya mazungumzo hayo imekamilika, lakini kutatua maswala yaliyobaki kunahitaji “uamuzi wa kisiasa”.

Mapema kabla ya hapo mwakilishi kwenye mazungumzo ya nyuklia wa Iran Bw. Abbas Araqchi amesema Marekani imekubali kuondoa sehemu kubwa ya vikwazo dhidi ya Iran, “lakini haitoshi”.