Mahali kilipozaliwa Chama cha Kikomunisti cha China pavutia watalii vijana
2021-05-17 18:38:49| cri

 

 

Idadi inayoongezeka ya vijana wa China wanaendelea kutembelea mahali ulipofanyika mkutano mkuu wa kwanza wa Chama cha Kikomunisti cha China, na eneo la makumbusho kuhusu chama hicho mjini Shanghai.

Mtafiti mshiriki kwenye eneo la makumbusho ya chama hicho Yang Yu amesema wastani wa umri wa walioshiriki kwenye mkutano wa kwanza taifa wa Chama cha Kikomunisti cha China ulikuwa miaka 28, na watu wa umri huo huo kwa sasa wameonesha hamasa ya kujua historia ya chama hicho.

Eneo la makumbusho linajulikana kwa jina la Shikumen, ambalo ni nyumba ya kawaida ya Shanghai yenye ua na lango la mawe. Nyumba hiyo imehifadhi mwonekano wake wa zamani, na kuwa sehemu moja inayovutia ya historia ya Chama cha Kikomunisti cha China.

Kwa mujibu wa takwimu, kabla ya mwaka 2017, nyumbani hiyo ilikuwa inapokea watalii kati ya laki 5 na laki 5.5 kwa mwaka, lakini mwaka 2018 ilipokea watalii milioni 1.42, na mwaka 2019 ilipokea watalii milioni 1.46. Kwa sasa nyumba hiyo itafunguliwa kabla ya Julai 1 baada ya ukarabati wa miezi mitano.