Jambo muhimu kwa sasa ni nchi zilizoendelea kuondoa vikwazo vya kuuza chanjo nje
2021-05-18 19:43:09| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, jambo muhimu kwa sasa ni nchi zilizoendelea ambazo zimenunua chanjo kwa wingi kuliko zinazohitaji, kuondoa vizuizi vya kuuzia chanjo nchi za nje, kuongeza utoaji wa chanjo, na kuziba uhaba wa chanjo katika nchi zinazoendelea.

Siku moja iliyopita China imetangaza kuacha hakimiliki za chanjo ya COVID-19. Bw. Zhao amesema, suala kuu la sasa ni namna ya nchi zinazoendelea kupata chanjo kwa usawa. Amesema China inatimiza ahadi yake ya kuifanya chanjo kuwa bidhaa ya umma duniani, na ingawa kiwango cha utoaji  wa chanjo nchini China ni kidogo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu, China inatoa mchango halisi kwa ajili ya nchi zinazoendelea kupata na kumudu chanjo, na kuendelea kutoa mchango huo.