Mkuu wa UM atoa wito wa juhudi zaidi kuzifanya teknolojia za kidijitali kuwa “nguvu ya kuleta mazuri”
2021-05-18 09:01:16| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana Jumatatu alitoa wito wa kuongeza juhudi ili kuzifanya teknolojia za kidijitali kuwa “nguvu ya kuleta mabadiliko mazuri”.

Kwenye ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mawasiliano ya Simu inayoadhimishwa Mei 17 kila mwaka, Bw. Guterres amesema juhudi za pamoja zinatakiwa kufanywa ili kuzifanya teknolojia za kidijitali kuwa nguvu ya kuleta mabadiliko chanya yanayosaidia kutimiza malengo ya Maendeleo Endelevu na kutoacha nyuma hata mtu mmoja.

Bw. Guterres pia amesema mpaka sasa watu bilioni 3.7, ikiwa ni karibu nusu ya watu wote duniani, wengi wao wakiwa ni wanawake, bado hawajaunganishwa kwenye mtandao wa Internet.