China kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya majumba ya makumbusho
2021-05-18 17:30:57| CRI

 

 

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mustakabali wa Majumba ya Makumbusho: Kufufuka na Kukarabati. Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Idara ya Mabaki ya Utamaduni ya Kale ya China, baada ya kushinda janga la COVID-19, China itaimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya majumba ya makumbusho, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa pamoja.

Naibu mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Majumba ya Makumbusho, ambaye pia ni naibu mkuu wa Shirikisho la Majumba ya Makumbusho ya China Bw. An Laishun, amesema kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho ya mwaka huu ina maana tofauti. Amesema,“Neno kufufuka lina maana wazi, yaani kufufua kazi za majumba ya makumbusho na mapato yake, na kurejesha hali ya kawaida. Neno kukarabati lina maana mbili. Moja ni kujenga upya sura ya kijamii ya majumba ya makumbusho, na nyingine ni kuwa na mawazo mapya.”

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, mwaka jana kutokana na janga la COVID-19, wastani wa wakati wa kufungwa kwa majumba ya makumbusho duniani ulikuwa siku 150, na mapato ya ujumla yalipungua kwa asilimia kati ya 40 na 60.

Kwa bahati nzuri, mwaka jana wastani wa wakati wa kufungwa kwa majumba ya makumbusho nchini China ulikuwa chini ya siku 30. Naibu mkuu wa Idara ya Mabaki ya Kale ya Utamaduni Bw. Guan Qiang amesema, ushirikiano wa kimataifa kati ya majumba ya makumbusho duniani ni muhimu sana, unaweza kuhimiza mawasiliano kati ya ustaarabu tofauti, na uchangia ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Amesisitiza kuwa majumba ya makumbusho ya China yanapaswa kuchambua, kutafiti, kuonesha na kueneza rasilimali za mabaki ya utamaduni ya kale, ili kuongeza ushawishi wa utamaduni wa China duniani. Amesema, “Kwanza, tunapaswa kuimarisha ubunifu na uratibu wa ngazi ya juu zaidi, na kutengeneza mipango ya muda wa kati na muda mrefu na mipango ya kila mwaka ya kufanya maonesho ya mabaki ya utamduni ya kale katika nchi za nje, ili kuonesha utamaduni wa China kwa pande zote. Pili, tunatakiwa kuongeza yaliyomo ya maonesho hayo, ili kuongeza mvuto na ushawishi wa mabaki ya utamaduni ya kale ya China.”