Jumuiya ya kimataifa yafuatilia kupamba moto kwa mgogoro kati ya Palestina na Israel
2021-05-18 09:44:05| CRI

Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali ya Gaza na kuongezeka kwa idadi ya vifo na majeruhi, na kuzisisitiza Israel na Palestina kusimamisha mapigano mara moja.

Mgogoro kati ya pande hizo mbili jana uliingia katika wiki ya pili na kusababisha vifo vingi vya raia na majeruhi wengi wakiwemo wanawake na watoto.

Jana alfajiri, ndege za kivita za Israel zilifanya shambulizi dhidi ya sehemu ya kusini ya Gaza, zikilenga mahandaki ya makundi yenye silaha kwenye eneo hilo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza kuwa kurudi kwenye meza ya mazungumzo ni njia pekee ya kumaliza mvutano kati ya pande hizo.