Serikali ya Biden yaidhinisha mauzo ya silaha kwa Israel yenye thamani ya dola za Marekani milioni 735
2021-05-18 19:19:43| CRI

Serikali ya Marekani imeidhinisha kuizuia Israel silaha zinazolenga kwa usahihi, na habari kutoka gazeti la Washington Post zinasema bunge la Marekani lilipewa taarifa kuhusu mpango huo tarehe 5 Mei, karibu wiki moja kabla ya kuanza kupamba moto kwa mgogoro kati ya Israel na wapiganaji wa kundi la Hamas.

Baada ya bunge la Marekani kupewa taarifa kuna muda wa siku 15 kwa bunge kuchukua hatua kama likitaka kupinga, na sasa zimebaki siku nne kwa bunge kufanya hivyo.

Baadhi ya wabunge kutoka Chama cha Democrat wameonyesha wasiwasi kuhusu mpango huo, wakati jeshi la Israel linaendelea kufanya mashambulizi kwenye ukanda wa Gaza, na kuwadhuru raia.

Jana Rais Joe Biden wa Marekani alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu, na kusema anaunga mkono pande hizo mbili kufikia makubaliano ya kusimamisha mapambano.