Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza nchini China atoa wito wa juhudi za kimataifa dhidi ya COVID-19
2021-05-18 09:09:41| CRI

Mtaalam mwandamizi wa magonjwa ya mfumo wa kupumua wa China Dkt. Zhong Nanshan ametoa wito wa mshikamano na ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na virusi vya Corona na kuzuia janga lingine.

Dkt. Zhong amesema mwezi Julai mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuanzishwa kwa Tume Huru ya Utayarishaji na Mwitikio kwa Maambukizi Makubwa (IPPPR) ili kutathmini mwitikio wa dunia kuhusu janga la virusi vya Corona chini ya uongozi wa Shirika hilo.

Tarehe 12 mwezi huu, Tume hiyo ilitoa ripoti yake, ikionyesha mapengo yaliyopo sasa na suluhisho kwa maeneo ya kipaumbele katika kuzuia janga hili. Ripoti hiyo pia imependekeza kuifanya chanjo ya virusi vya Corona kuwa bidhaa ya afya ya umma, na kuongeza kuwa nchi zenye kipato kikubwa zinapaswa kuchangia kwenye mradi wa COVAX, unaolenga kuziwezesha nchi zenye kipato cha chini na cha kati kupata chanjo hiyo.