Jeshi la Israel lafyatulia risasi kikosi cha doria cha Lebanon kusini mwa Lebanon
2021-05-19 08:51:26| CRI

Jeshi la Israel limewafyatulia risasi askari wa kikosi cha doria cha Lebanon karibu na uzio wa mpakani kwenye Kivuko cha Al-Manara kusini mwa Lebanon. Mpaka sasa hakuna ripoti za vifo au majeruhi kwenye tukio hilo.

Tangu Israel ianze kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas Jumatatu wiki iliyopita, watu 213 kwenye maeneo ya Palestina yaliyozingirwa wameuawa, wakiwemo watoto 61.