Marais wa China na Russia washuhudia uzinduzi wa miradi ya ushirikiano ya nishati ya nyukilia
2021-05-19 20:10:56| CRI

 

 

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin leo wameshuhudia hafla ya uzinduzi wa miradi ya ushirikiano ya nishati ya nyukilia, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya nyukilia vya Tianwan na Xudabao.

Huu ni mwaka wa 20 tangu nchi hizo mbili zisaini Makubaliano ya Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki. Hii ni mara ya kwanza kwa marais hao kufanya mawasiliano kwa njia ya video kwa mwaka huu, na hii ina maana muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili.