China kufungua jumba la makumbusho la Chama cha Kikomunisti cha China
2021-05-19 19:53:39| CRI

 

 

Idara ya taifa ya urithi wa utamaduni ya China (NCHA) imesema jumba la makumbusho la Chama cha Kikomunisti cha China litafunguliwa hivi karibuni mjini Beijing.

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo inasema kuanzia mwezi Juni mwaka huu, jumba hilo litafanya maonyesho kuhusu historia ya Chama cha Kikomunisti cha China. Mbali na jumba hilo, makumbusho kuhusu mkutano mkuu wa kwanza wa taifa wa Chama cha Kikomunisti cha China yatafunguliwa mjini Shanghai.

Hadi sasa China ina jumla ya majumba ya makumbusho zaidi ya 1,600 na maeneo ya kumbukumbu kuhusu historia ya mapinduzi. Kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2020 majumba hayo yamefanya maonyesho zaidi ya 4,000.