Bunge la Russia lapitisha mswada wa kuondoa mkataba wa anga wazi
2021-05-19 19:27:34| CRI

Baraza la chini la bunge la Russia leo limetangaza kuwa, wabunge wote wa baraza hilo wamepitisha mswada uliotolewa na rais Putin wa nchi hiyo kuhusu kuondoa “mkataba wa anga wazi”. Taarifa hiyo inasema, Russia kujiondoa kwenye mkataba huo kunatokana na Marekani kuvunja mkataba huo kwa upande mmoja. Mwezi Novemba mwaka jana, Marekani ilitangaza kujitoa kwenye mkataba huo.