Wabunge wa Iran watoa taarifa ya pamoja kuisisitiza Marekani kuondoa vikwazo vyote dhidi ya nchi hiyo
2021-05-19 09:26:47| CRI

Wabunge 200 wa bunge la Iran jana walitoa taarifa ya pamoja wakisema, Marekani kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Iran ni sharti muhimu kwa Iran kurejesha utekelezaji wake wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Taarifa hiyo imesema, Marekani na nchi nyingine za magharibi bado hazijaonesha nia thabiti ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran kutokana na maendeleo ya mazungumzo yaliyofanyika huko Vienna. Wabunge hao wamesema mazungumzo kati ya Iran na nchi nyingine yatapata mafaniko endapo Iran itapata maslahi halisi ya kiuchumi kutokana na makubaliano ya JCPOA.