China inakaribia kuzifikia nchi zilizoendelea katika kiwango cha utoaji wa chanjo ya virusi vya Corona kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata chanjo hiyo katika wiki za karibuni nchini humo.
Shirika la Habari la Reuters limesema, kama China itaendelea na kiwango cha utoaji chanjo cha kila siku kilichoko sasa, nchi hiyo itatoa chanjo kwa asilimia 87 ya idadi ya watu wake mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamati ya Afya nchini China, jumla ya dozi milioni 406.938 za chanjo ya Corona zimetolewa China bara wakati nchi hiyo ikiongeza kasi ya utoaji wa chanjo hiyo.