Mkuu wa UM ataka wanawake, vijana, na chanjo ya COVID-19 vijumuishwe katika ufufukaji baada ya COVID-19
2021-05-20 09:22:53| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kujumuishwa kwa wanawake na vijana, na upatikanaji wa chanjo ya virusi vya Corona katika mipango ya ufufukaji baada ya janga hilo barani Afrika.

Akizungumza kwanye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Amani na usalama barani Afrika hapo jana, Guterres amezitaka nchi wanachama kufanya juhudi chanya kujumuisha wanawake na vijana wakati zikiandaa mipango ya ufufukaji baada ya janga hilo.

Amesema kuhakikisha fursa sawa, ulinzi wa jamii, upatikanaji wa rasilimali na huduma na ujumuishi pamoja ushirikishwaji wa uhakika katika kutoa maamuzi, sio tu ni wajibu wa kisheria na kimaadili, bali ni sharti muhimu la nchi kuondokana na vurugu, na kuingia kihalisi kwenye njia ya amani na maendeleo endelevu.