Rais wa Marekani na waziri mkuu wa Israel wafanya tena mazungumzo kwa njia ya simu
2021-05-20 09:46:21| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu kwa njia ya simu na kusema anatarajia mgogoro kati ya Palestina na Israel unamalizika.

Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikisema, rais Bieden aliitarajia kuwa pande hizo mbili zitasimamisha vita, lakini taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel ilisema, Bw. Netanyahu aliishukuru Marekani kwa kuunga mkono haki ya Israel ya kujilinda, na kuongeza kuwa Israel itaendelea na operesheni za kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Habari nyingine kutoka wizara ya ulinzi ya Marekani zinasema, waziri wa ulinzi Marekani Bw. Lloyd Austin siku hiyo alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Israel Bw. Benjamin Gantz, akisisitiza kumaliza mgogoro kati ya Palestina na Israel.