China yatoa pendekezo la kiwenzi la kuunga mkono maendeleo ya Afrika
2021-05-20 19:40:17| CRI

China yatoa pendekezo la kiwenzi la kuunga mkono maendeleo ya Afrika_fororder_微信图片_20210520190526

Mkuu wa idara ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wu Peng leo amefanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi kwenye mjadala wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu “kuhimiza ukarabati wa Afrika baada ya janga la COVID-19, na kuondoa kiini cha migogoro” ameshirikiana na nchi za Afrika kutoa pendekezo la kiwenzi la kuunga mkono maendeleo ya Afrika.

Amesema pendekezo hilo linaunga mkono ukarabati na ufufukaji baada ya janga la COVID-19, kuonyesha vya kutosha ufuatiliaji kwa Afrika, na lina ishara wazi ya masikilizano na ushirikiano wa kunufaishana. China na Afrika zinakaribisha nchi na mashirika ya kimataifa hasa wenzi wa jadi wa ushirikiano wa Afrika kujiunga kwenye pendekezo hilo, na kuunga mkono kwa pamoja maendeleo ya Afrika.