Ushirikiano wa nishati ya nyuklia kati ya China na Russia wapongezwa
2021-05-20 09:47:33| cri

 

 

     Rais Xi Jinping wa China na rais Vladmir Putin wa Russia jana wameshuhudia kwa njia ya video sherehe ya kuzinduliwa kwa miradi ya ushirikiano wa nishati ya nyuklia kati ya nchi hizo mbili, inayojumuisha kituo cha umeme wa nyuklia cha Tianwan na kituo cha umeme wa nyuklia cha Xudabao.

Jamii ya kimataifa imeona kuwa, ushirikiano huo kati ya China na Russia umeonesha imani na majukumu ya nchi hizo mbili katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza matumizi ya nishati safi na kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa duniani.

      Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nishati la kimataifa Fatih Birol amesema, China ni nchi muhimu inayohimiza matumizi ya nishati endelevu, na ni muhimu sana kwake kufanya ushirikiano na nchi nyingine, na kuhimiza utafiti kwa pamoja.