China yatarajia kundi la G20 kutekeleza zaidi jukumu la mwitikio wa misukosuko duniani
2021-05-20 18:58:11| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, China inatarajia mkutano wa afya duniani utakaofanyika kesho, utahimiza jukumu la kundi la G20 katika kukabiliana na misukosuko wa dunia.

Bw. Zhao amesema hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona yameongezeka tena duniani. China inatarajia kundi hilo kuendelea kuongoza ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na janga hilo, kutoa msimamo imara wa kushikilia mfumo wa pande nyingi na kusukuma mbele mshikamano ili kuleta imani na nguvu katika kushinda mapambano dhidi ya janga la COVID-19 na kuboresha usimamizi wa afya duniani.

Habari zinasema rais Xi Jinping wa China atashiriki kwenye mkutano huo kwa njia ya video.