China yazitaka pande zote kuhimiza mchakato wa kurejesha utekelezaji wa Mkataba wa Nyukilia kati ya Marekani na Iran
2021-05-20 09:31:52| Cri

Mkutano wa duru mpya ya maofisa waandamizi wa kisiasa wa Tume ya pamoja ya Mkataba wa Nyuklia wa JCPOA unaendelea huko Vienna, Austria, ambapo mwakilishi wa China katika mazungumzo hayo Bw. Wang Qun alihudhuria.

Bw. Wang amesema, hivi sasa mazungumzo kati ya Marekani na Iran juu ya kurejesha utekelezaji wa mkataba huo kwa ujumla yamepata maendeleo, lakini bado kuna safari ndefu kabla ya kutimiza lengo la kufikia makubaliano. Amesema pande zote zinazohusika zinapaswa kuongeza juhudi na kuhimiza mpango wa pande zote na wenye ufanisi wa utekelezaji. Ili kutimiza lengo hilo, China pia inatumai kuwa Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) zitaweka mipango kwa wakati kuhusu kuongeza muda kwa “Makubaliano ya muda ya kiufundi kati ya pande mbili”.

Habari nyingine zinasema, Rais wa Iran Hassan Rouhani jana Jumatano alisema, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika siku kadhaa zilizopita yamepata maendeleo makubwa, na kwamba kutokana na uvumilivu na upinzani wa Iran, Iran imeifanya Marekani ikiri “makosa yake”.