Baraza la Usalama lapitisha taarifa ya mwenyekiti kuhusu ukarabati wa Afrika baada ya janga
2021-05-20 09:48:11| cri

 

 

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana ameendesha mkutano wa ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliokuwa na kaulimbiu “amani na usalama barani Afrika: kuhimiza ukarabati wa Afrika baada ya janga na kuondoa vyanzo vya migogoro”, na washiriki wa mkutano huo wamepitisha taarifa ya mwenyekiti iliyotolewa na China, ambayo ni mwenyekiti wa zamu wa Baraza hilo.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, janga la COVID-19 limeleta athari kubwa kwa sekta za uchumi, siasa, usalama na masuala ya kibinadamu barani Afrika, pia limeongeza migogoro barani humo. Taarifa hiyo imesema jumuiya ya kimtaifa inapaswa kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuonesha umuhimu mkubwa wa Umoja wa Mataifa, na kufanya uratibu katika kukabiliana na suala hilo.