Wapiganaji 12 wa Taliban wauawa kwenye mashambulizi ya anga nchini Afghanistan
2021-05-20 09:10:12| CRI

Wapiganaji 12 wa kundi la Taliban wameuawa jana Jumatano kwenye mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la anga la Afghanistan dhidi ya maficho ya kundi hilo mashariki mwa mkoa wa Laghman. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi hilo, mashambulizi hayo yalifanywa jana adhuhuri kwenye eneo la Salo, wilaya ya Ali Shing, na baadhi ya silaha za Taliban pia ziliteketezwa. Mpaka sasa kundi la Taliban bado halijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulizi hilo.