China kutoa msaada wa kibinadamu wa dharura kwa Palestina
2021-05-21 19:56:14| CRI

 

 

Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Maendeleo la China Bw. Tian Lin, amesema China itatoa msaada wa kibinadamu wa dharura kwa serikali ya Palestina katika muda mfupi iwezekanavyo.

Bw. Tian amesema ili kuisaidia serikali ya Palestina na watu wake kukabiliana na msukosuko wa kibinadamu na kuonyesha moyo kibinadamu wa kimataifa, serikali ya China imeanzisha utaratibu wa kimataifa wa mwitikio wa kibinadamu.

Bw. Tian amesema serikali ya China itaipatia serikali ya Palestina msaada wa dharura wa kibinadamu kulingana na mahitaji ya haraka ya Wapalestina kwa haraka iwezekanavyo, ili kuisaidia nchi hiyo kuwatibu watu walioumia na kuwapatia makazi wanaokosa makazi.