Mwakilishi wa China atoa wito kwa jamii ya kimataifa kubeba majukumu makubwa zaidi kwa utatuzi wa suala la Palestina
2021-05-21 09:00:07| Cri

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kubeba majukumu makubwa zaidi kwa Baraza la Usalama katika juhudi za kutatua suala la Palestina.

Bw. Zhang pia ametoa wito wa kumaliza uhasama na vurugu mara moja ili kuepusha majeruhi zaidi ya raia, na kuzitaka pande zinazohusika kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa na kulinda haki na maslahi halali ya watu wa Palestina .

Habari nyingine zimesema kuwa, Kundi la Hamas la Palestina limethibitisha kuwa limefikia makubaliano ya kusimamisha vita na Israel. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema, baraza la usalama la nchi hiyo limekubali kupokea makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa kwa kuratibiwa na Misri.