China yatoa waraka wa “Ukombozi wa Amani, Maendeleo na Ustawi wa Tibet
2021-05-21 19:57:09| CRI

China yatoa waraka wa “Ukombozi wa Amani, Maendeleo na Ustawi wa Tibet_fororder_VCG211143251343

Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka wa  “Ukombozi wa Amani, Maendeleo na Ustawi wa Tibet”, na kusema tangu Tibet ikombolewe, imepata maendeleo makubwa, na ina mustakabali mzuri.

Waraka huo unasema tarehe 23 Mei 1951, Makubaliano ya Njia ya Kuikomboa Tibet kwa Amani yalisainiwa kati ya serikali kuu ya China na serikali ya mkoa wa Tibet, na Tibet ilitangazwa kukombolewa rasmi.

Waraka huo unasema chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa Tibet wa makabila mbalimbali walifanya mageuzi, na kukomesha mfumo wa watumwa wa kilimo. Katika miaka iliyopita, uchumi wa sehemu hiyo umeendelea kwa kiasi kikubwa na maisha ya watu pia yameboreshwa sana.