China yatumai Ulaya itafikiria zaidi kusimamisha mkataba wa uwekezaji kati ya pande hizo mbili
2021-05-21 19:48:06| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China inatumai Ulaya itafikiria zaidi kuhusu kusimamisha mkataba wa uwekezaji kati ya China na Ulaya, kufanya uamuzi sahihi unaoendana maslahi yao wenyewe.

Bw. Zhao amesema Umoja wa Ulaya bila kujali malalamiko na upinzani wa China, umefanya uamuzi wa makosa kwa mujibu wa uongo na habari zisizo sahihi, kuingilia kati mambo ya ndani ya China, kukiuka sheria ya kimataifa na kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa, na kuharibu vibaya uhusiano kati ya China na Ulaya.

Bw. Zhao amesema China ina nia ya dhati ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Ulaya, pia itashikilia kulinda mamlaka yake, usalama na maslahi ya maendeleo. Kuweka vizuizi na kupambana hakusaidii utatuzi wa suala hilo, pia siyo njia ya kutendeana kwenye uhusiano wa kiwenzi na kimkakti wa pande zote. Mazungumzo na ushirikiano ni njia sahihi.