Rais wa Marekani asaini mswada wa kupinga uhalifu wa chuki dhidi ya waasia
2021-05-21 11:06:33| Cri

Rais Joe Biden wa Marekani jana kwenye Ikulu alisaini mswada wa kupinga uhalifu wa chuki dhidi ya waasia wakati wa janga la COVID-19, na kuufanya mswada huo uwe sheria rasmi.

Rais Biden amesema, tangu mwaka mmoja uliopita, wamarekani wengi wenye asili ya waasia walikumbwa na janga la COVID-19 na chuki, ambapo wanaishi kwenye hofu na wasiwasi. Kukabiliwa na uhalifu wa chuki, kukaa kimya tu pia ni kuunga mkono uhalifu. Amewataka raia wawe na mshikamano na kupinga uhalifu wa chuki na ubaguzi wa rangi.