Watu mashuhuri wa nchi mbalimbali wampongeza rais Xi Jinping kwa hotuba yake kwenye mkutano wa kilele wa afya duniani
2021-05-22 15:13:30| cri

Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria kwa kupitia video mkutano wa kilele wa afya duniani. Hotuba aliyotoa kwenye mkutano huo imepongezwa na watu mashuhuri wa nchi mbalimbali, ambao wanaona, wakati binadamau wanapokabiliana na maambukizi ya COVID-19, kipaumbele ni kujenga dunia yenye mustakabali wa pamoja katika mambo ya afya, na China inatenda kwa hatua madhubuti wazo hilo.

Mkurugenzi wa Kiini cha utafiti wa China cha Nigeria Bw. Charles Onunaiju alisema, hotuba ya rais Xi Jinping inalingana na matakwa ya jumuiya ya kimataifa ya kufanya ushirikiano ili kukukabiliana na virusi vya Corona, pia inaonyesha kuwa China ina nia imara katika kuchangia ujenzi wa dunia yenye mustakabali wa pamoja katika mambo ya afya. Alieleza matumaini yake kuwa, Afrika na China zitaweza kupanua wigo wa ushirikiano katika fani ya afya.

Rais Xi kwenye hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kutatua maswala ya uzalishaji na mgawanyo wa chanjo za virusi vya Corona ili nchi zinazoendelea zinaweza kupata na kumudu chanjo hizo. Mtaalamu wa Kenya wa masuala ya uhusiano wa kimataifa Bw. Cavince Adhere alimpongeza rais Xi kwa maelezo hayo, akisema China imetoa ufadhili wa chanjo kwa nchi nyingi za Afrika, hatua ambayo inaonyesha kwamba China inashikilia kuwa pamoja na Afrika katika kukabiliana na shida.