Iran yasema IAEA haliwezi kupata data ya video kuhusu usimamizi wa zana za nyuklia za Iran
2021-05-24 08:57:57| CRI

 

 

Spika wa bunge la Iran Bw. Muhammad Baqir Qalibaf, amesema kutokana na kumalizika kwa makubaliano ya kiufundi ya muda wa miezi mitatu kati ya Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) na Iran, shirika hilo haliwezi kupata data ya video kuhusu usimamizi wa zana za nyuklia za Iran.

Ofisa mmoja amesema, makubaliano kati ya IAEA na Iran huenda yakarefushwa kwa mwezi mmoja zaidi kwa masharti fulani. Katika kipindi hicho kama matakwa ya Iran yatatekelezwa, data ya video kuhusu usimamizi zitakabidhiwa kwa shirika hilo.