Iran yasema itaendelea kurikodi data za shughuli zake za nyuklia kwa mwezi mmoja tu
2021-05-24 20:15:08| Cri

Balozi wa Iran na mwakilishi wa kudumu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) lenye makao yake makuu mjini Vienna Kazem Gharibabadi amesema Iran imelitaarifu shirika hilo kwamba itaendelea kurikodi data za shughuli zake za nyuklia kwa mwezi mwingine mmoja tu.

Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, akijibu kauli zilizotolewa na mwenzake wa Marekani Antony Blinken, amesema kwenye twitter kwamba kuondoa vikwazo vilivyowekewa Iran na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ni jukumu la kisheria na kimaadili la nchi hiyo. Jana Jumapili alipohojiwa kwenye televisheni, Blinken alisema haijafahamika kama Iran iko tayari kufanya kila liwezekanalo kufuata tena makubaliano ya nyuklia (JCPOA). Bw. Zarif ameonya kwamba kuishinikiza Tehran kwa kuiwekea vikwazo ili kufikia makubaliano haikufanikiwa wakati wa Trump na haitafanikiwa hivi sasa.