China yafanya ibada ya kumuaga “baba wa mpunga chotara” Yuan Longping
2021-05-24 17:47:09| Cri

Leo China imefanya ibada ya kumuaga Bw. Yuan Longping, ambaye anajulikana kama “baba wa mpunga chotara” aliyefariki Jumamosi.

Licha ya kwamba leo ni siku yenye pilika za kazi, maelfu ya watu waliovalia mavazi meusi walijitokeza na kuweka maua kwenye eneo hilo kabla ya ibada kuanza saa nne asubuhi huko Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Hunan. Mwanasayansi bingwa wa mpunga, aliyelima mpunga wa kwanza chotara alifariki dunia baada ya viungo vya ndani kushindwa kufanya kazi akiwa na umri wa miaka 91 huko Changsha. Mtaalamu huyo wa kilimo aliisaidia China kuleta maajabu makubwa na kulisha karibu moja ya tano ya watu duniani kwa kutumia chini ya asilimia 9 ya ardhi ya kilimo duniani.

Mwaka 2019, Bw. Yuan alitunukiwa medali ya Jamhuri, ambayo ni tuzo ya heshima kubwa ya China.