China kuendelea kuzihimiza Palestina na Israel kuanzisha tena mazungumzo ya amani
2021-05-24 20:09:20| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China itaendelea kufanya kazi yake ya kiujenzi katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuzihimiza Palestina na Israel kuanzisha tena mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo.

Bw. Zhao Lijian amesema, China ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa mwezi huu katika baraza la usalama, imeshirikiana na Norway, Tunisia na Ufaransa kutoa pendekezo la kutoa taarifa ya mwenyekiti kuhusu kusimamisha vita kati ya Palestina na Israel, na kuhimiza nchi wanachama wote kupitisha pendekezo hilo.

Habari zinasema, baraza la usalama limeafikiana na kupitisha taarifa ya mwenyekiti kuhusu kusimamisha vita kati ya Palestina na Israel.