Marais wa China na Iran wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
2021-05-25 10:08:22| CRI

 

 

Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani kwa njia ya simu, na kupongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona, na kuhimiza ushirikiano. Rais Xi amesema China inatilia maanani uhusiano kati yake na Iran, na inapenda kushirikiana na Iran katika kuimarisha ushirikiano katika sekta zote.

Rais Rouhani amesema Iran inapenda kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na China, na kupanua ushirikiano wa kunufaishana kwenye sekta za uchumi na nishati, na kuhimiza ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.