Mkurugenzi mkuu wa WHO asema bado haijagundulika aina mpya ya virusi vya Corona inayoathiri chanjo
2021-05-25 19:38:22| Cri

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema katika ufunguzi wa Mkutano wa 74 wa Afya duniani kuwa, hadi sasa, bado haijaguduliwa aina mpya ya virusi vya Corona ambayo inaweza kuathiri chanjo, upimaji na matibabu.

Bw. Ghebreyesus amesema hata hivyo hakuna uhakika kuwa aina mpya za virusi vya Corona hazitatokea katika siku za baadaye, na maambukizi ya virusi hayatamalizika hadi hali ya maambukizi itakapodhibitiwa katika nchi zote duniani. Pia ameitaka jamii ya kimataifa ishirikiane kadiri iwezavyo, kutoa chanjo kwanza kwa watu wenye hatari kubwa zaidi kuambukizwa wakiwemo watumishi wa afya na wazee.