Abiria 213 wajeruhiwa baada ya treni za chini ya ardhi kugongana Kuala Lumpur, Malaysia
2021-05-25 10:08:53| CRI

 

 

Treni mbili za chini ya ardhi zimegongana jana usiku huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, na kusababisha abiria 213 kujeruhiwa, 47 kati yao wamejeruhiwa vibaya. Hivi sasa abiria wote wa treni hizo wameokolewa na kukimbizwa hospitali.

Waziri mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yasin amesema kazi ya kipaumbele kwa sasa ni kuwaokoa na kuwatibu majeruhi, na kuziagiza wizara ya mawasiliano na kampuni ya taifa ya ujenzi wa miundombinu kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.