China yazitaka pande mbalimbali ziimarishe ulinzi wa viumbe anuwai
2021-05-25 09:30:00| cri

 

 

Ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika husika ya kimataifa hivi karibuni ulifanya kwa pamoja kongamano kwa njia ya video, la kuadhimisha Siku ya kimataifa ya viumbe anuwai inayoadhimishwa Mei 22 kila mwaka.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, kongamano hilo lilizitaka pande mbalimbali zichukue hatua za dharura, kukabiliana na changamoto za kupungua kwa anuwai za viumbe, kuharibika kwa mazingira na kubadilika kwa tabianchi, na kujenga jumuiya ya binadamu na mazingira ya asili yenye mustakbali wa pamoja.