China kuendelea kushirikiana na pande mbalimbali kulinda usalama wa wafanyakazi wa kulinda amani
2021-05-25 19:45:37| CRI

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China ikiwa nchi mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na nchi inayotuma askari wengi zaidi wa kulinda amani, itaendelea kushirikiana na pande mbalimbali, kuhimiza kulinda usalama wa askari wa kulinda amani, na kuipa umuhimu operesheni ya kulinda amani kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa dunia.

Bw. Zhao Lijian amesema, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha taarifa ya mwenyekiti kuhusu usalama wa askari wa kulinda amani, kutoa maagizo mapya katika kutimiza kulifanya baraza hilo lipitishe mada ya usalama wa walinzi wa amani kuwa utaratibu, kutoa chanjo kwa askari wa kulinda amani, na kutumia teknolojia mpya ili kuhakikisha usalama wa askari hao.

Bw. Zhao Lijian amesema, operesheni ya kulinda amani ni njia muhimu ya kulinda amani na usalama wa kimataifa. Hivi sasa, hatari zinazowakabili askari wa kulinda amani zinaongezeka. Kupitisha taarifa hiyo kunaonyesha maafikiano mapya ya baraza la usalama katika kulinda usalama wa askari wa kulinda amani chini ya hali mpya.