Mkuu wa UM atoa wito wa mageuzi ya sekta uchimbaji madini kuelekea maendeleo endelevu
2021-05-26 08:52:48| CRI

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kufanywa mageuzi kwenye sekta ya uchimbaji wa madini ili kuunga mkono maendeleo endelevu na mchakato wa kuelekea uchumi wa kijani.

Akiongea kwenye mkutano wa mtandaoni kuhusu mageuzi ya sekta ya madini kwa ajili ya maendeleo endelevu, Bw. Guterres amesema jumuiya ya kimataifa ina jukumu la pamoja la kuhakikisha raslimali za madini zinanufaisha watu wote, na pia inatakiwa kuhifadhi mazingira ya asili kwa ajili ya vizazi vijavyo.