Umoja wa Ulaya wasonga mbele kutimiza lengo la kufanikiwa kupambana na janga la COVID-19
2021-05-26 18:15:42| cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen amesema, Umoja huo unasonga mbele kutimiza lengo la kufanya asilimia 70 ya watu wazima wa Umoja huo kupata chanjo kabla ya mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Baada ya kushiriki kwenye mkutano maalum wa Umoja huo, Bibi von der Leyen amesema, ifikapo wikiendi ijayo, nusu ya watu wazima wa Umoja huo watapata chanjo.

Taarifa iliyotolewa na mkutano huo imesema, umoja huo utaendelea kujitahidi kuongeza uwezo wa utengenezaji wa chanjo ili kukidhi mahitaji ya dunia. Pia umeahidi kutoa dozi zaidi ya milioni 100 za chanjo kwa nchi zinazohitaji zaidi.