China yasema jumuiya ya kimataifa haikubaliani na uamuzi wa Japan wa kumwaga baharini majitaka ya kinyukilia
2021-05-26 10:30:38| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, amesema uamuzi wa Japan wa kutupa baharini majitaka ya kinyukilia utaathiri vibaya vizazi na mazingira ya dunia, na jumuiya ya kimataifa haikubali vitendo hivyo vya Japan.

Bw. Zhao ameitaka Japan itambue majukumu yake kwenye suala la majitaka yenye mionzi yaliyochaguliwa katika kituo cha umeme wa nyuklia cha Fukushima, kurudi kwenye njia ya mazungumzo na wadau na mashirika husika ya kimataifa, na kutoanza operesheni ya kumwaga baharini majitaka ya kinyuklia.