Mpatanishi wa Iran asema mazungumzo ya Vienna yanaweza kupatiwa ufumbuzi
2021-05-26 18:19:55| Cri

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi jana Jumanne alisema hana uhakika kama mazungumzo yanaweza kuhitimika kwenye duru mpya ya mazungumzo ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) lakini amesisitiza kwamba kuna uwezekano.

Amebainisha kuwa kwenye raundi iliyopita waliweza kupiga hatua muhimu kwenye mazungumzo yao, lakini bado kuna masuala muhimu ya kutatuliwa. Naye msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei mapema Jumanne alisema Iran na washiriki wengine wa mazungumzo hayo wamefikia makubaliano ya awali juu ya namna ya kuokoa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.