Jeshi la Afghanistan lawaua wapiganaji 162 wa Taliban
2021-05-26 08:53:20| CRI

 

 

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan inasema, katika saa 24 zilizopita jeshi la serikali limewaangamiza wapiganaji 162 wa kundi la Taliban na kuwajeruhi wengine 129 kwenye operesheni zilizofanyika katika mikoa mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jeshi la serikali lilivamia gereza moja la kundi la Taliban katika mkoa wa Herat na kuwaokoa wafungwa 41, wakiwemo askari 19.