Rais wa China asisitiza kuimarishwa kwa sayansi na teknolojia katika ngazi ya juu
2021-05-28 20:17:56| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuongeza juhudi katika ujenzi wa China kuwa nchi inayoongoza katika sayansi na teknolojia na kutimiza kujitegemea katika sayansi na teknolojia na kujiimarisha katika ngazi ya juu zaidi.

Rais Xi amesema hayo leo alipohutubia mkutano mkuu wa wajumbe wa Akademia ya Sayansi ya China, Akademia ya Uhandisi ya China na wajumbe wa Shirikisho la Sayansi na Teknolojia la China.