Rais Xi Jinping ampongeza Bashar kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Syria
2021-06-01 10:25:45| Cri

Rais Xi Jinping wa China amempongeza Bashar al-Assad kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Syria.

Kwenye pongezi zake, rais Xi amesema China na Syria zina urafiki wa jadi na Syria ni moja ya nchi za kiarabu zilizoanzisha mapema uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China. Yeye anazingatia sana kukuza uhusiano kati ya China na Syria na anapenda kufanya juhudi pamoja na rais Bashar, kutumia fursa inayotokana na maadhimisho ya miaka 65 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili ili uhusiano kati ya China na Syria upate maendeleo makubwa zaidi.

Amesisitiza kuwa China inaunga mkono mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi ya Syria, na inapenda kutoa usaidizi kwa Syria kupambana na virusi vya Corona, kufufua uchumi na kuboresha maisha ya watu.