Watatu wameuawa katika tukio la ufyatuaji wa risasi katika sherehe ya mahafali huko Florida, Marekani
2021-06-07 09:20:57| CRI

Shirika la utangazaji la Marekani ABC limesema watu zaidi ya watatu wameuawa na wengine zaidi ya sita wamejeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi liliotokea katika sherehe ya mahafali kwenye kaunti ya Miami-Dade, Florida, kusini mashariki mwa Marekani.

Mkuu wa idara ya polisi ya Miami-Dade Bw. Freddy Ramirez amesema milio ya risasi ilisikika saa nane usiku, wakati magari mawili yakiegeshwa katika kituo cha maduka ambako sherehe ya mahafali ilikuwa inafanyika kwenye mgahawa.

Ameongeza kuwa mtu mmoja aliyekuwa ndani ya gari aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakiondoka. Mwanamke mmoja na wanaume wawili wameuawa, huku wanaume watatu na wanawake watatu wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitalini.