Biden afanya mazungumzo na rais wa Ukraine kabla ya mkutano na mwenzake wa Russia
2021-06-08 09:23:29| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani amesisitiza tena uungaji mkono wa nchi hiyo kwa Ukraine, alipofanya mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa njia ya simu, ikiwa hatua ya kuondoa mashaka ya Ukraine kabla ya mkutano kati ya viongozi wa Marekani na Russia utakaofanyika baadaye mwezi huu.

Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Bw. Jake Sullivan, amesema rais Biden amemwambia Bw. Zelensky kuwa Marekani italinda kithabiti mamlaka, ukamilifu wa ardhi na matumaini ya Ukraine, huku akitarajia rais Zelensky atafanya ziara nchini Marekani katika majira ya joto mwaka huu.

Bw. Sullivan amesema Marekani inauchukulia mkutano wa kilele kati ya viongozi wa Marekani na Russia kama fursa ya mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, lakini nchi hiyo haina matarajio makubwa na mkutano huo.